
Klabu ya Paris Saint-Germain ndiyo timu pekee iliyotumia fedha nyingi kusajili duniani baada ya kutua kwa Kylian Mbappe kutoka Monaco kunafanya kikosi chao cha kwanza XI kuwa cha thamani ya euro 640milioni.
Zaidi ya euro 418milioni zimetumika kuwanunua wachezaji wanne tu msimu huu 2017 (Yuri Berchiche, Dani Alves, Neymar na Mbappe), Les Parisiens imeusambaratisha utaji wa Russia uliotumia kununua nyota wa Monaco katika miaka ya karibuni.
Neymar alinunulia wa euro 222milioni kutoka Barcelona uhamisha uliotikisa dunia kutokana na dau hilo kubwa.
PSG
imepiga bao lingine kwa kumnyakuwa Mbappe kwa mkopo wa muda mrefu na
wanategemea kulipa euro 180milioni msimu ujao na kumchukua moja kwa
moja.
Ni kipa pekee Alphonse Areola na Adrien Rabiot
waliopatikana kupitia akademi ya miamba hiyo ya Ligue 1 huku Alves
akiwasiri kutoka Juventus akiwa mchezaji huru.
Pamoja
na mabeki wengine Thiago Silva na Marquinhos, wote walinunua kutoka ligi
ya Italia ‘Serie A’ kwa euro 42milioni na euro 31.5milioni, huku beki
wa kushoto Layvin Kurzawa akichukuliwa kwa euro 25milioni.
Marco
Verratti alinunuliwa euro 12 milioni kutoka Pescara huku Angel Di Maria
akiwaghalimu euro 63milioni kutoka Manchester United.
- Areola: Academy (2012)
- Dani Alves: Huru (Juventus, 2017)
- Thiago Silva: euros 42m (Milan, 2012)
- Marquinhos: euros 31.5m (Roma, 2013)
- Kurzawa: euros 25m (Monaco, 2015)
- Verratti: euros 12m (Pescara, 2012)
- Di María: euros 63m (United, 2015)
- Rabiot: Academy (2012)
- Neymar: euros 222m (Barcelona, 2017)
- 10.Cavani: euros 64.5m (Napoli, 2013)
- Mbappe: euros 180m italipwa msimu ujao (Monaco, 2017)
0 comments:
Post a Comment