Tuesday, September 5, 2017

Picha ya pamoja Idris Sultani na Ben Breaker

Staa maarufu hapa bongo anayetambulika kwa jina la Idris Sultan kutokea ukurasa wa instagram ameeleza changamoto zote alizopitia na rafiki yake ambaye ni mwanamitindo anafahamika kwa jina Ben Breaker alinukuliwa akiandika hivi,From day 1 you've always been a brother, tumetembea kilombero mpaka masai camp mara kibao, tumekula bablishi dukani kwenu kidogo mtaji ukate, tumeazimana viatu sana maana kiko kimoja tu cha kutokea, Beatus katuokoa sana mia na mia mbili za kupanda basi kwenda complex kuongea na watoto wa kishua ili tujue kiingereza, nakumbuka nilikua sichezi namba 9 bila wewe kuwa 7 timu ya mtaani tukafukuzwa na visu sinoni kwa kina Joh makini kisa tumewafunga, tumetoboa kwa skonzi moja na soda ndogo za saifi miaka, tumesoma kwa shift ya mchana na jioni Arusha seki, nimekuja kupiga kitabu weekend pugu weekend maana mlikua nondo physics hatari, tumenunua nguo sokoni pale soko kuu kila jioni kwenye mikokoteni ili tuende na fashen 😂.. Naomba nieleweke hizi kwangu ni memory nzuri sana za jinsi nilivyokuja kua Idris mnayemuona. Kitabu kitanoga kwa mikiki sio kwa utekezi mwanzo mwisho. Hali yako ni mapito tu labda uamue kubaki ulipo ☺️👌🏽 cc: @ben.breaker 

0 comments:

Post a Comment