Kimbunga kikali kinachoitwa Irma kimesababisha uharibifu mkubwa katika eneo la Caribbean ambapo takribani ya watu saba wameuwawa, pia zaidi ya nusu ya wakazi hawana umeme baada ya kimbunga Irma kusababisha mvua kubwa na upepo mkali.
Pia kisiwa kidogo cha Barbuda kinasemekana kukumbwa na uharibifu mkubwa hadi kutajwa kuwa kisichoweza kukalika huku maafisa wakionya kuwa himaya ya Uingereza ya St. Martin imeharibiwa na kimbunga hicho.


0 comments:
Post a Comment