Dele Alli alifunguka kupitia ukurasa wake wa Twitter - ''Kuyaweka
bayana, ishara hiyo ilikuwa ni ya utani kati yangu na rafiki yangu Kyle
Walker,'' ''Naomba msamaa kwa kosa lolote lililotendeka.''
Shirikisho
la kandanda duniani (Fifa) linasubiri ripoti kutoka kwa viongozi wa
mechi hiyo, inayotarajiwa kutolewa mwishoni mwa wiki, kabla ya kutoa
maamuzi iwapo kumfungulia mchezaji mashtaka kwa ukosefu wa nidhamu au
la.
Hapo awali ilionekama ishara hiyo iliyofanywa na Alli kwa
Turpin ambaye alioneka wakibadilishana maneno alipokuwa akitolewa
uwanjani katika dakika 93 ya mchezo. Alli na beki Walker walikuwa wakiichezea klabu ya Spurs hadi pale Walker alipojiunga na Manchester City majira ya joto.
Meneja wa Uingereza Gareth Southgate amesema wawili hao , walikuwa
''wanachokozana,'' aliongeza '' wako na njia za kushangaza kama njia ya
mawasiliano yao.''
Hasira ya Alli hapo awali ilizuwa wasiwasi.
Alikosa
mechi ya kuwania taji la ligi ya Premia 2015-16 baada ya kumpiga kofi
mchezaji wa Bromwich Albion, Claudio Yacob, na alitolewa uwanjani kwa
kufanya kosa jingine dhidi ya kiungo wa Gent Brecht Dejaegere wakati wa
mechi ya ligi ya bara ulaya mwezi Febrauri iliyopita.
Uingereza
ilianza mechi yao vibaya siku ya Jumatatu , kupitia bao la Stanislav
Lobotka alilolifunga katika dakika tatu ya mchezo. Eric Dier alisawazisha baada ya mpira kupigwa kutoka kwa kona, kabla Marcus Rashford kufunga na kuiongozea makali timu yake.
Uingereza wako kileleni na alama tano, mbele ya Slovakia katika kundi F wakiwa bado wamesalia na michezo miwili. Mshindi
katika makundi atafuzu moja kwa moja kwa kombe la dunia msimu ujao
litakaloandaliwa huko Urusi, huku watakao kuwa katika nafasi ya pili
wakicheza mechi za marudiano.
0 comments:
Post a Comment