![]() |
| BEN POL
"Mama
you are the Best!.. Wakati Baba anafungwa gerezani Keko alikuacha na ujauzito wangu (yaani mimi nikiwa tumboni mwako nna miezi 6) na ulikuwa na mtoto mkubwa wa miaka miwili Marehemu #michael #mybrother #Rip , tukiishi kwenye nyumba za kupanga Vingunguti, ulipambana, uliuza maandazi, uliuza vitumbua ilimradi kuhakikisha wanao tunakula vizuri, ulifanikiwa kunizaa mimi salama salmini (Nilizaliwa Nyumbani, si Hospitali) ukanilea nikakua, hapo baadae Baba akaachiwa huru na kunikuta nimeshakuwa "Jibaba" lakini zote ni juhudi zako, nakuombea heri mama yangu, mwenyezi mungu akuweke na akupe furaha kila siku, #SioniAibu .. Naipenda sana hii Stori Yangu, ulinihadithia wewe mwenyewe Mama yangu, wewe ni Soldier!!.. Mungu akubariki na awabariki wamama wote duniani.. |
Monday, September 4, 2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

0 comments:
Post a Comment