Wednesday, September 6, 2017



Mfanyabiashara Yusuph Manji ambaye pia ni Diwani wa kata ya Mbagala Kuu amevuliwa Udiwani leo baada ya kushindwa kuhudhuria vikao vya kamati ya maendeleo ya halmashauri na vikao vya barazala madiwani.


Hayo yamezungumzwa na Meya wa Manispaa ya Temeke Abdalah Chaurembo leo alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari ambapo amesema wamefanya hivyo kutokana na Manji kutohudhuriwa vikao zaidi ya 6.

"Tumesha mwandikia Waziri wa Tamisemi George Simbachawene kuhusu suala hilo ili aweze kuijulisha Tume ya uchaguzi na kupanga uchaguzi mwingine" ameeleza hayo Meya Chaurembo.

Hata hivyo amesema kuanzia leo Yusuph Manji sio Diwani tena wa Kata ya Mbagala Kuu kwa sababu amepoteza sifa kwa mujibu wa sheria ya Tamisemi na amewaomba wakazi wa mbagala kuu wawe watulivu wakati wakisubiri kupata

0 comments:

Post a Comment