Mwenyekiti
wa New Life In Christ Mkoani Kilimanjaro, Bi. Elly Makyao (kulia)
akikabidhi misaada ya kibinadamu ya Wafungwa waliopo Magerezani nchini
kwa Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, Dkt. Juma Malewa. Hafla fupi
ya Makabidhiano ya Misaada hiyo imefanyika leo Septemba 08, 2017 katika
Viwanja vya Gereza Kuu Karanga – Moshi, Mkoani Kilimanjaro.
Kamishna
Jenerali wa Magereza Nchini, Dkt. Juma Malewa akitoa hotuba fupi wakati
wa hafla ya kupokea misaada ya kibinadamu kwa Wafungwa waliopo
Magerezani iliyotolewa na Asasi ya "New Life In Christ" leo Septemba 08,
2017 katika Viwanja vya Gereza Kuu Karanga - Moshi, Mkoani Kilimanjaro.
Mkurugenzi
wa Doricas Aide International - Tawi la Tanzania, Bi. Lilian Urasa
akitoa maelezo mafupi namna Shirika linavyoshirikiana na Serikali katika
Nyanja mbalimbali hapa nchini.
Aina
mbalimbali ya misaada ya kibinadamu iliyotolewa kwa Wafungwa waliopo
Magerezani nchini na Asasi ya "New Life In Christ". Hafla ya
Makabidhiano ya misaada hiyo imefanyika leo Septemba 08, 2017 katika
Viwanja vya Gereza Kuu Karanga, Moshi ambapo Mgeni rasmi alikuwa ni
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa.
Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa akiwakabidhi cheti cha
shukrani Viongozi wa Asasi ya "New Life In Christ" kwa kutambua mchango
wao kwa niaba ya Jeshi la Magereza Tanzania na Serikali kwa ujumla.
Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa akimsukuma askari ambaye
ameketi kwenye Baiskeli Maalum ya kubebea wagonjwa wasiojiweza ambayo ni
miogoni mwa vifaa mbalimbali vilivyotolewa kama msaada kwa Jeshi la
Magereza na Asasi ya "New Life In Christ"(kushoto) ni Mkurugenzi wa
Doricas Aide International anayeshughulikia Miradi ya Afya katika nchi
za Africa, Bi. Mirjam Verwij.
Baadhi
ya Wakuu wa Magereza waliohudhuria hafla hiyo wakifuatilia kwa umakini
hafla ya tukio hilo kama inavyoonekana katika picha.
Mkuu
wa Magereza Mkoani Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza,
Julius Sangu’udi(wa kwanza kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa Magereza
Mkoa Tanga, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, John Masunga na
Mkuu wa Magereza Mkoani Morogoro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa
Magereza, Ramadhani Nyamka kama inavyoonekana katika picha.
Wafungwa
wa Kike wa Gereza Kuu Karanga, moshi wakionesha mikate na skonsi
zinazotengenezwa na wafungwa wa Kike katika gereza hilo ikiwa ni sehemu
ya utekelezaji wa programu mbalimbali za urekebishaji magerezani.
Kamishna
Jenerali wa Magereza Nchini, Dkt. Juma Malewa(katikati) akiwa katika
picha ya pamoja Askari wa Magereza Mkoani Kilimanjaro(waliosimama)
pamoja na Viongozi Wawakilishi wa Asasi ya "New Life In Christ" mara
baada ya kupokea misaada ya kibinadamu ya Wafungwa waliopo Magerezani
nchini (wa kwanza kushoto) ni Mwenyekiti wa New Life In Christ Mkoani
Kilimanjaro, Bi. Elly Makyao(wa pili kushoto) ni Mratibu wa Huduma za
Magereza toka Asasi ya "New Life In Christ", Bw. Charles Shang'aa (wa
pili kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Arusha, Kamishna Msaidizi
Mwandamizi wa Magereza, Khamis Nkubasi( wa tatu kulia) ni Mkuu wa
Magereza Mkoani Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza,
Hassan Mkwiche (Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
0 comments:
Post a Comment