Monday, September 4, 2017



WEKENI FEDHA BENKI NA KOPENI FEDHA KWA MALENGO - RC Makalla
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla amewataka wananchi kuwa na utamaduni wa kuweka Fedha benki na pia wanapokopa Fedha benki wakope kwa malengo
- Hayo ameyasema leo wakati wa ufunguzi wa Tawi la NMB Uyole . Amewataka wananchi wasikope fedha kwa malengo YA biashara badala yake wanatumia ktk matumizi mengine ikiwemo uchangiaji sherehe mbalimbali au ununuzi wa zamani za ndani
- Amewahamasisha wananchi kuweka Fedha benki badala YA kuhifadhi kwenye viroba majumbani kwani kufanya hivyo inahatarisha usalama wao na Fedha
Ameipongeza Benki YA NMB kwa kuwa na huduma Nzuri, mtandao mkubwa nchini kwa kuwa na matawi 207 na kati YA HAyo matawi 10 yamefunguliwa ktk Mkoa wa Mbeya
- Amewaeleza wananchi kuwa serikali ina hisa asilimia 32 ktk benki YA NMB na mwaka huu serikali imepata gawio la shilingi bilioni 16.5




















0 comments:

Post a Comment