Posted by Williammalecela.com on Wednesday, September 06, 2017
*WANANCHI WAFURIKA KUPIMA AFYA BURE VIWANJA VYA MNAZI MMOJA*
Zoezi la *Upimaji wa Afya Bure* kwa Muda wa Siku Tano limeanza leo
kwenye Viwanja vya *Mnazi Mmoja* ambapo baadhi ya Wananchi wamewahi
kwenye Viwanja hivyo tokea *saa 10 Usiku.* Mwamko huu ni baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam *Paul Makonda* kutangaza zoezi la Upimaji bila Malipo.
*Madaktari bingwa na Wauguzi* kutoka Hospital za Umma,Jeshi na zile za
Watu Binafsi wanaendelea na zoezi la Upimaji kwa Wananchi. Katika
Upimaji huo Mwananchi atakaepimwa na kubainika kuwa na matatizo ya
kiafya atapelekwa Hospital na kupatiwa *Matibabu Bure.*
0 comments:
Post a Comment