Tuesday, September 5, 2017





*MUFTI WA TANZANIA AMTEMBELEA RC MAKONDA*

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa *Paul Paul C. Makonda* leo ametembelewa Ofisini kwake na *Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zuber* na kufanya Mazungumzo.

Katika Mazungumzo hayo *Mufti* amemtia Moyo *Makonda* na kumsihi asikate tamaa sababu kazi anayoifanya ni *Njema* na inagusa watu wa makundi yote hususani Wanyonge.


Aidha *Mufti* amemuunga mkono *RC Makonda* kwa kumletea mdau atakaejenga Ofisi za Walimu kwenye *Shule tatu.*

*"Nimeona nisikae kimya ndio maana nimeona niunge mkono Kampeni yako ya Ujenzi wa Ofisi za Walimu kwa kutafuta mdau ambae atajenga Ofisi kwenye Shule Tatu ili Walimu wafanye kazi kwenye mazingira mazuri"* Alisema Mufti.

*Makonda* amemshukuru *Mufti* kwa kumtembelea na kusema kuwa ataendelea na jitiada zake za kufanya kazi kwa bidii ilikutatua changamoto za Wakazi wa Dar es salaam.

Aidha *Makonda* amewaomba Viongozi wa *Dini na Vyama vya Siasa* kujitoa kwa pamoja ili kuijenga Dar es Salaam.








0 comments:

Post a Comment