Wednesday, September 6, 2017

Image result for simba scMshambuliaji wa Simba, Mohammed Ibrahim ‘Mo Ibra’ amesema sasa wapo tayari kuivaa Azam na kulipiza kisasi cha msimu uliopita.


Simba na Azam zitakutana katika mchezo wa Ligi Kuu Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Uhuru, huku Simba ikiwa na kumbukumbu ya kufungwa kwenye mchezo wa mwisho uliozikutanisha timu hizo.
 Image result for mohamed ibrahim wa simba
Mo Ibrahim alisema kwa sasa kikosi cha Simba kina njaa ya mafanikio na itakuwa vigumu kuziacha pointi tatu watakapokutana na Azam.
“Tuna timu nzuri iliyokamilika, kukosa mabao ni sehemu ya mpira. Tunakwenda kujirekebisha kabla ya kucheza na Azam,”alisema Mo ambaye alifunga bao pekee katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Fa iliyozikutanisha timu hizo, Mei mwaka huu.
 
Jumapili iliyopita, Simba ilicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Hardrock ya Pemba na licha ya kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 washambuluaji Laudit Mavugo na Juma Liuzio walikosa mabao mengi ya wazi.
Kocha Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja alisema Simba itafanya vizuri kwenye mchezo wa Azam kwakuwa baadhi ya wachezaji wake muhimu watakuwa wamerudi kikosini.
“Wanasimba wawe watulivu, kila mchezaji aliyesajiliwa ana nafasi yake. Niyonzima, Okwi na Juuko tumewakosa leo, lakini ni wachezaji muhimu. Kujiandaa kwetu ni kuhakikisha tunashinda kila mchezo,”alisema Mayanja, akiwatetea washambuliaji wake.
Categories:

0 comments:

Post a Comment