Sunday, September 10, 2017

Msanii wa filamu za bongo ambaye ni maarufu kwa kucheza sehemu za michambo Riyama Ally, ametoa siri ya kudumu kwenye mahusiano yake na mumewe ambaye wengi walimpinga kwa kuwa amemzidi umri Leo My, na kusema kuwa alichukulia udhaifu wake na kuukubali.

Riyama amesema mwanzoni alipata changamoto kubwa hususan kutoka kwa mashabiki wake, lakini aliamua kutulia na mwenzi wake huyo, huku akichukulia mapungufu yake na kuyakubali, na hatimaye kuweza kufikia hatua ya kufunga ndoa takatifu.
Riyama amesema iwapo mtu yeyote atachukulia mapungufu ya mwenzake, kuvumilia na kuheshimiana, ndiyo silaha kubwa ya kudumu kwenye mahusiano bila kuzingatia umri, na sio kubadili wenza kwa sababu tu ana kasoro fulani, kwani hakuna aliye mkamilifu.

0 comments:

Post a Comment