Polisi Mkoani Geita wanamshikilia kijana Samson Petro (18) mkazi wa Katoro wilayani Geita kwa tuhuma za kuteka watoto katika mikoa ya Arusha na Geita.
Akithibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo Kamanda wa polisi mkoani Geita, Mponjoli Mwabulambo amesema kuwa jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi na utakapokamilika atafikishwa Mahakamani.
Kamanda Mwabulambo amesema kijana huyo alikamatwa usiku wa Septemba 2 usiku katika nyumba ya kulala wageni ya Shitungulu iliyopo mji mdogo wa Katoro akiwa na mtoto Justine Ombeni mwenye umri wa miaka miwili aliyetekwa Ijumaa siku ya Eid El Haji mkoani Geita.
Amesema mtuhumiwa alimficha mtoto huyo katika chumba namba 11 cha kulala wageni iitwayo Shitungulu wakati akisubiri mpango wake wa kutaka alipwe shilingi milioni nne na wazazi wa mtoto huyo Omben Mshana na Elizabeth Omben.
0 comments:
Post a Comment