Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe Stephen Kebwe, ameagiza kukamatwa mara moja na kurejeshwa nchini mwao raia watatu kutoka China wanaodaiwa kuwepo nchini bila kibali na kuendesha shughuli za uchimbaji wa madini katika eneo la Maseyu Morogoro.
Dkt. Kabwe ametoa maagizo hayo jana kufuatia agizo alilopewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Septemba 2, 2017 wakati akiongea na viongozi na watumishi wa kiwanda cha Philp Morris kinachotengeneza sigara aina ya Marlboro katika ziara yake ya kukagua maendeleo ya viwanda mkoani Morogoro. Ambapo alipata taarifa kuwepo wa raia wa China wanaondesha shughuli za uchimbaji wa madini aina ya mabo bila ya kuwa na kibali.
Malalamiko hayo yaliwasilishwa na Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki Mheshimiwa Omary Mgumba kuwa wawekezaji hao kutoka China wanaendesha shughuli za uchimbaji wa mabo katika kijiji cha Maseyu wilayani Morogoro bila ya kuwa na kibali cha kufanya kazi hiyo.
Hivyo baada ya Mkuu wa mkoa kubaini ukweli katika hilo ametoa amri raia hao kukamatwa mara moja na kurejeshwa nchini kwao China kutokana na kukiuka utaratibu na kubainika kuwepo nchini na kuendesha shughuli zao bila ya kuwa na vibali.
0 comments:
Post a Comment