Friday, September 1, 2017



Lemutuz.com kuanzia hivi sasa itakuwa ni sehemu sahihi zaidi kwako kupata taarifa mbalimbali za michezo kutoka katika kila pande ya dunia kwa muda na wakati sahihi. Utapata tetesi zote za usajili barani Ulaya na Kuangalia michezo mbalimbali mubarashara 'LIVESTREAMING' katika simu, tablet au Computer yako.

Ungana na Lemutuz.com hapa chini kupata taarifa rasmi kuhusiana na dirisha la usajili majira ya joto barani Ulaya:
 

 
Klabu ya PSG ilifanikiwa kuinasa saini ya mshambuliaji hatari Keylian Mbappe Lotin kwa mkopo wa muda mrefu huku katika mkataba kukiwa na kipengele cha nyota huyo kununuliwa kwa Paundi Milioni 190. (Chanzo: PSG & AS MONACO)


Mshambuliaji wa kihispaniola aliyekuwa anaitumikia klabu ya Swansea City hapo jana aliikacha Chelsea Fc na kujiunga na klabu ya Tottenham Hotspurs kwa kusaini kandarasi ya miaka 2. (Chanzo: )
 
Klabu ya Chelsea Fc baada ya kumkosa beki Alex Sandro hapo jana walifanikiwa kuinasa saini ya beki kutoka Lazio, Muitaliano Davide Zappacosta huku akisaini mkataba wa miaka 4 kuitumikia klabu hiyo.(Chanzo: )
 
Nikukumbushe tu dirisha la usajili nchini Hispania halijafungwa, huku likitarajiwa kufungwa leo hiii usiku, hivyo basi bado kuna uwezekano wa Diego Costa kuelekea Atletoc Madrid na Philippe Coutinho kujiunga na FC Barcelona. (Chanzo: )


Hapo jana mshambuliaji hatari wa Ivory Coat, Wilfried Bony alikamilisha uhamisho kutoka Stoke City kujiunga na klabu yake ya zamani Swansea City baada ya kusaini kandarasi ya miaka 2. (Chanzo: )

Leicester City ilifanikiwa kuinasa saini ya kiungo Aleksandar Dragović kutoka Bayern Leverkusen kwa mkopo wa muda mrefu. (Chanzo: )

Hapo jana mushkeri mkubwa ulikuwa kwenye dili lililomhusisha Ross Barkley mwenye thamani ya £35m, baada ya Everton kukubaliana kila kitu na Chelsea, Barkley alibadili mawazo na kukataa kujiunga na timu hiyo na kupelekea dili hilo kutokamilika. (Chanzo: SkySports)


Huko Itali klabu ya Inter Milan ilifanikiwa kuinasa saini ya Yann Karamoh kutoka klabu ya Caen kwa mkopo wa miaka miwilihuku kukiwa na kipengele cha kumnunua. (Chanzo: )

Klabu ya Everton ilikamilisha usajili wa Nikola Vlašić kwa £10m kutoka klabu ya Hajduk Split kwa mkataba wa miaka 5.(Chanzo: )

Mshambuliaji wa klabu ya Arsenal Lucas Perez alifanikiwa kujiunga na klabu ya DeportivoL Coruna kwa mkopo wa muda mrefu. (Chanzo: )

 
Kiungo Danny Drinkwater alikamilisha uhamisho wa kujiunga na klabu ya Chelsea akitokea Leicester City kwa mkataba wa miaka 5 huku dili hilo likigharimu £35m. (Chanzo: )

Endelea kutembelea www.lemutuz.com kwa taarifa mbalimbali za michezo hususan tetesi za usajili barani ulaya na kutazama michezo mbalimbali 'MUBASHARA' ikiwemo Ligi Kuu zote barani Ulaya na Michuano ya Ligi Mabingwa barani Ulaya
Categories:

0 comments:

Post a Comment