Tottenham italazimika kumpatia beki wa kati Toby
Alderweireld, 28, mapato mapya yalioimarika ama imwachilie kuhamia klabu
nyengine kulingana na mshauri wa mchezaji huyo. (Het Nieuwsblad via
Daily Telegraph)
Kiungu wa kati wa Chelsea Eden Hazard amemtaka mshambuliaji Diego
Costa kutafuta suluhu ya kuhakikisha kuwa ataichezea tena klabu
hiyo.Costa mwenye umri wa miaka 28 hajaichezea timu hiyo msimu huu baada
ya kukataa kurudi katika mazoezi. (Marca via Daily Mirror)
Arsenal
inajaribu kuanzisha mazungumzo ya kandarasi za wachezaji ambao mikataba
yao inakamilika mwisho wa msimu ujao ili kuzuia tatizo kama lile la
msimu huu ambapo wachezaji kama vile Alexis Sanchez na Mesut Ozil
walianza msimu wakiwa wamesalia na kandarasi ya mwaka mmoja kila
mmojawao. (Daily Telegraph)
Mkurugenzi mkuu wa klabu ya Arsenal Ivan Gazidis amewatumia ujumbe
wachezaji wa timu hiyo akiwaambia kwamba kikosi chao kilichoimarika
kinaweza kugombea taji la Uingereza msimu huu.(Daily Star)
Mkufunzi
wa Celtic Brendan Rodgers anasema kuwa klabu hiyo itakuwa imevunja
rekodi yake ya uhamisho itakapomsajili Patrick Robert kwa kandarasi ya
kudumu lakini Manchester City haitaki kumuuza mchezaji huyo mwenye umri
wa miaka 20 kwa kitita cha £30m. (Goal)
Manchester United sio klabu isiojulikana iliowasilisha ombi la kutaka
kumsajili winga wa Leicester Riyadh Mahrez mwenye umri wa
miaka(Leicester Mercury)
Kiungo wa kati wa Everton Ross Barkley
hakujiunga na Chelsea katika siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho kwa
sababu simu ya mkufunzi wa Chelsea Antonio Conte ilipuuziliwa mbali
wakati mwakilishi wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 alipotaka
kuzungunmza jukumu lake kulingana na mchezaji wa zamani wa Manchester
CityJoey Barton. (Talksport)
Winga wa Everton Kevin Mirallas
mwenye umri wa miaka 29 amekasirika baada ya klabu hiyo kumkataza kurudi
klabu yake ya zamani Olympiakos (Daily Mirror)
Juventus iko
tayari kumnunua beki wa Napoli Faouzi Ghoulam ambaye amevivutia vilabu
vya Chelsea na Liverpool (Tuttosport via Talksport)
0 comments:
Post a Comment