Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) imesema kuwa deni la Tsh 424 trilioni
inayoidai Migodi ya Bulyanhulu Gold Mine (BGML) na Pangea Minerals
(PML) inayoendeshwa na Acacia limekokotolewa na wataalamu wa kodi
waliobobea waliokuwa miongoni mwa wajumbe wa kamati mbili za kuchunguza
makinikia zilizoteuliwa na Rais Magufuli.Akizungumza kwenye mahojiano
maalumu na gazeti la MTANZANIA jana, Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala
wa TRA, Gerald Mwanilwa alisema, Deni la Acacia halikuja kibahati mbaya,
lilikokotolewa na wataalamu wabobezi wa masuala ya kodi tangu (BGML na
PML) walipoanza kukwepa kodi hadi tulipobaini jambo ambalo limesababisha
deni kuonekana kubwa.” Afisa huyo alisema kwamba, wote wanaodhani TRA
imezikomoa kampuni hizo kwa kuzipa deni hilo, wanakosea kwa sababu deni
hilo limetokana na malimbikizo ya ukwepaji kodi.Taarifa iliyotolewa
kwenye tovuti ya Acacia baada ya kupata madai hayo ya TRA ilionyesha
kuwa deni hilo la USD 190 bilioni, BGML wanadaiwa USD 154 bilioni na PML
wakidaiwa USD 36 bilioni.
Katika
USD 190 bilioni, USD 40 bilioni ni malimbikizo ya kodi na USD 150
bilioni zikiwa ni riba na faini kutokana na kukiuka sheria.
0 comments:
Post a Comment