Msanii mkongwe wa Muziki, Z Anto ameingia studio na kurekodi wimbo maalumu kwaajili ya kumuombea afya njema Mbunge wa Singida kupitia tiketi ya Chadema, Tundu Lissu aliyelazwa nchini Kenya baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwake Area D, Dodoma muda mchache akitokea Bungeni.
"Nimeguswa sana na hili suala la Mhe. Tundu Lissu na nikiwa kama mzalendo ninayeitakia mema nchi yangu nimeona ni bora nitoe nyimbo kwa ajili ya kuwakumbusha na kuwasisitiza watanzania wenzangu tuendelea kumuombea dua Mhe. Lissu", amesema Z Anto.
Amefunguka na kudai ameguswa na tukio lililompata Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu la kupigwa risasi na watu wasiofahamika hivyo ameamua kuachia nyimbo kwa lengo la kuwakumbusha watanzania kudumish
a amani pamoja na kumuombea Lissu.
Pamoja na hayo, Z Anto ameendelea kwa kusema "ikiwa wabunge kwa pamoja waliweza kutoa nusu ya posho zao za kikao cha siku kimoja kuweza kumsaidia Lissu kwa ajili ya matibabu nami kwa upande wangu nikaona siyo vibaya kutoa nyimbo kama sehemu ya mchango kwake ili kwa pamoja watanzania tuungane kumuombea dua kwa sababu tukio lilimtokea siyo la kawaida. Huu wimbo siyo wa kisiasa wala chama fulani ila ni wa kila mtanzania", amesisitizia Z Anto.
Kwa upande mwingine, Z Anto amewataka wasanii wenzake wawe na moyo wa uzalendo kwanza ili kuweza kudumisha na kutangaza amani ya nchi.

0 comments:
Post a Comment