Mara baada ya Uhuru kupokwa ushindi, Lowassa alifanya mahojiano na Azam Tv na kuahidi kwenda tena nchini Kenya kumpigia kampeni Uhuru, endapo angemuhita.
Hata hivyo wikiendi hii alifanya tena mahojiano na Gazeti la Jamhuri na kudai kuwa, Mahakama Kuu ya Kenya imetoa haki kwa watu (NASA) waliokuwa njiani kuporwa haki yao.
Kwa Hali hiyo, Lowassa na CHADEMA wanajua fika kwamba Uhuru alikuwa amepoka haki ya Odinga. Sasa Lowassa kwa nini anataka tena kumpigia kampeni mtu aliyeiba kura, huku wao ndio huwa wanalalamika kuwa, kura zao ziliibwa mwaka 2015.
Ni aibu kuwa, wafuasi na vyombo vya habari vinavyotetea wapinzani, wamekomalia kusifia sijui Uhuru wa Mahakama nchini Kenya na kusahau issue muhimu "wizi wa kura."
Wapinzani wameanza kumtupa mkono kidogokidogo baada ya Uhuru kutishia kuwashughulikia majaji waliotoa maamuzi hayo. Dah!! hata ndiyo ya "Mgema akisifiwa, tembo hutia maji;" na "Aisifuye mvua imemnyea."
0 comments:
Post a Comment