Monday, September 4, 2017

 Image result for Lwandamina
Kocha Mkuu wa mabingwa watetezi Ligi Kuu Tanzania bara Yanga Sc, George Lwandamina, ametua tangu usiku wa kuamkia jana akitokea kwenye msiba wa baba yake. 

Baada ya kurejea nchini kocha huyo ameiambia klabu hiyo iongeze mtaalamu mwingine kwenye benchi la ufundi huku washambuliaji wake watatu; Obrey Chirwa, Amissi Tambwe na Geofrey Mwashiuya, walikuwa na majeruhi kwa muda mrefu wakiuguza tatizo la aina moja, maumivu ya magoti.
Lwandamina amethibitisha ameomba kutafutiwa mtaalamu wa matibabu ya viungo atakayesaidiana na daktari wa timu hiyo Dk. Edward Bavu.

Mmoja wa viongozi wa  Yanga alisema tayari maombi hayo ambayo hata wao wameyakubali, yameshaanza kufanyiwa kazi kwa kumtafuta mtaalamu huyo kwa kuangalia ndani na nje ya nchi atakayefanya kazi hiyo.

Lwandamina alisema: “Nikweli nimewaomba wanitafutie huyo mtu, sawa sasa tuna daktari wa timu lakini tunatakiwa sasa kufikiria mbali zaidi kumaliza hali kama hii ya kuwa na wachezaji wengi muhimu majeruhi kama hivi na hili linaweza kuwa tatizo zaidi unapokuwa katika mashindano makubwa ya Afrika ambayo hayana muda wa kupoteza kila mchezo ni muhimu.”
Categories:

0 comments:

Post a Comment