Wednesday, September 6, 2017


Kumekua na tatizo la  upungufu wa maziwa  kwa wanawake wanao nyonyesha  hivyo ziko njia ambazo zinaweza kuongeza uzalishaji wa maziwa.


Mama anae nyonyesha anaweza kupika Uji wa pilipili manga amabo ni mwepesi  na kunywa mara 2 kwa siku ambapo  ni asubuhi na jioni.

Njia ingine ni mbegu za maboga,  Mama anae nyonyesha anaweza kuzitafuna au kuchanganya kwenye uji na hata  chai ambapo anaweza kunywa mara mbili kwa kwa siku.

Hata hivyo anaweza kutengeneza  Juice ya karoti na kchanganya na tangawizi kisha  kunywa mara 2 kwa siku

Aidha Tende pia ni   njia nzuri kwa  kutafuna vipande vi 3 -4 kwa  siku au kutoa mbegu ndani ya tende na kusaga kwenye blenda kisha  kuchanganya na maziwa fresh  na kunywa mara 2 kwa siku.

Lakini pia Supu ya samaki au nyama iliyo changanywa na mboga mboga inaweza kusaidia ikiwa pamoja na  Maji ya kunywa ni muhimu zaidi kunywa kwa wingi.

0 comments:

Post a Comment