AGIZO la Serikali la kupiga marufuku ngoma ya kigodoro, linaoenekana kupuuzwa na kikundi hicho, kimekuwa kikitoa burudani huku ikiambatana na vitendo vya kihalifu kama kawaida.Wakizungumza na Fullshangwe kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, baadhi ya wakazi wa jiji hilo, walisema wanashangaa kuona vikundi hivyo vikiendelea kutoa burudani katika mitaa mbalimbali bila ya kuchukuliwa hatua.Mussa Khamisi, ambaye ni kazi wa Mtaa wa Jitegemee, Mabibo Makutano, alisema juzi zilitokea vurugu wakati moja ya vikundi hivyo, kilipokuwa kikitoa burdani ya sherehe ya kumtoa mtoto baad ya kutimiza siku 40 (beseni), tangu kuzaliwa.
Alisema sherehe hiyo ilifanyika kwa mmoja wa wakazi wa mtaa huo, aliyefahamika kwa jina la Mchika, ambako kundi kubwa la vijana waliokuwa wakivuta bangi na dawa za kulevya kuanzisha vurugu za kutaka kuwabaka wasichana na kuiba.
Khamis, alisema baada ya kutokea vurugu hizo, mshereheshaji (MC), alilitahadharisha kundi hilo la wahalifu kwa kuwataka waache vurugu kwa kuwa walikuwa na vibali kisheria vilivyowaruhusu kuitisha ngoma hiyo.
“Tulishangaa kusikia kuwa walikuwa na kibali kwa sababu awali tulisikia kuwa ngoma hizo zimepigwa marufuku sasa sijui nani aliyewapatia kibali hicho,”alihoji Khamis.
Mohamed mnyambe, Mkazi wa Minazini, Mwananyamala, alisema wanaliomba jeshi la polisi kuongeza ulinzi katika eneo hilo kutokana vikundi vya uhalifu vinavyoandamana na ngoma hiyo kuongezeka kila kukicha.
Alisema, hivi sasa mtaa huo umekuwa na usalaama mdogo kutokana na hata vikundi vya ulinzi shirikishi kushindwa kuwadhibiti wahalifu hao ambao wanawafanya wakazi wa eneo hilo kushindwa kutembea zaidi ya saa 1:00 usiku
Akizungumzia vikundi hivyo Mei 27 mwaka huu, Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum, Suleiman Kova, alisema vikundi vya ngoma za kigodoro, kangamoko, mnanda, mchiriku, baikoko na nyingine ambazo zinachezwa usiku katika maeneo kadhaa jijini Dar es Salaam, zimepigwa marufuku.
Kwa mujibu wa Kova, polisi imebaini vijana wanaojihusisha na vikundi vya uhalifu vilivyojiita majina ya Mbwa Mwitu, Panya Road, Bad Face, Machizi Sabini na Wadudu wa Dampo hupenda kushiriki katika ngoma aina hiyo, ambazo kwa kawaida huchezwa hadi usiku wa manane.
0 comments:
Post a Comment