Asernal imefuzu kucheza fainali za kombe la UEFA kwa
msimu wa 17 mfululizo baada ya kuichabanga Besiktas ya Uturuki kwa jumla
ya goli 1-0.
Mchezaji wa Arsenal(kushoto) akipambana na mchezaji wa Basiktas(kulia). Arsenal ilishinda 1-0
Katika mchezo wa awali wiki moja iliyopita, timu hizo zilitoka sare ya kutofungana.
Hata hivyo, mchezaji mpya aliyejiunga na Arsenal msimu huu, Alexis Sanchez ndiye
aliyeiwezesha Asernal kusonga mbele baada ya kufunga goli la kwanza
tangu ajiunge na Arsenal akitokea Barcelona mwezi mmoja uliopita.
Sanchez aliyenunuliwa kwa kitita cha pauni milioni 35 kutoka Barcelona
kwa kipindi chote cha mchezo alihaha kutafuta goli, ambapo katika dakika
moja ya nyongeza katika kipindi cha kwanza cha mchezo aliweza
kutumbukiza kimiani goli pekee kwa Arsenal na kufuzu kutoka hatua ya
makundi kucheza fainali za UEFA kwa mwaka huu
Arsenal ilipata nafasi za kumaliza mchezo mapema, lakini wachezaji
wake Santi Cazorla na Alex Oxlade-Chamberlain walipoteza nafasi nyingi
za wazi walizopata.
Zikiwa zimebaki dakika 15 kumaliza mchezo
kipindi cha pili, Arsenal ilipata pigo baada ya mlinzi wake wa kulia
Mathieu Debuchy alitolewa nje kwa kadi nyekundu kutokana na kuonyeshwa
kadi mbili za njano. Lakini Arsenal waliendelea kupambana hadi dakika ya
mwisho ya mchezo.
Timu nyingine zilizofuzu kucheza fainali za UEFA
kwa mwaka huu katika michezo ya Jumatano usiku ni Athletic Bilbao
iliyopata ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Napoli. (Jumla 4-2), Bayer 04
Leverkusen 4, FC Copenhagen 0, jumla(7-2).
Ludogorets Razgrad 1 - 0 Steaua Bucharest
Malmö FF 3 - 0 FC Red Bull Salzburg
0 comments:
Post a Comment