Kocha wa Manchester United Louis van Gaal amewaudhi wapenzi wa klabu
hiyo baada ya kusema kuwa hakushangazwa na kichapo cha mabao 4-0
mikononi mwa klabu ya daraja la kwanza MK Dons katika mechi ya kuwania
ubingwa wa kombe la Capital One
Sikushangaa kulazwa4-0 na MK Dons
Man U ilibwagwa nje ya kipute hicho baada ya kushindwa katika mechi tatu za kwanza akiwa mkufunzi.
mimi sishangazwi na matokeo hayo kwa sababu najua kilichofanyika
''Timu haijengwi kwa mwezi mmoja''
Milton Keynes walicheza vizuri sana na pia walikuwa na bahati nzuri walipofika mbele ya lango
Katika mechi hiyo Jonny Evans alifanya makosa na kumruhusu Will Grigg kufungua mvua hiyo ya mabao
Grigg alifanya mambo kuwa mawili kwa nunge kunako dakika ya 60 ya
kipindi cha pili kabla ya mchezaji wa Arsenal aliyeko huko kwa mkopo
Benik Afobe kufuma mabao mawili na kuzamisha matumaini yeyote ya Man U
kukomboa mechi hiyo.
Van Gaal alisema kuwa alikuwa anataka kujua
uwezo wa kikosi chake cha pili haswa baada ya sare ya 1-1 dhidi ya
Sunderland wikiendi iliyopita
Nilikuwa nawajaribu wachezaji wetu wa timu ya pili
"nilibadilisha mfumo na nikawataka wachezaji mtu mmoja mmoja iliniweze kusaili uwezo wao lakini unaona kilichotokea .''
''Tulicheza vyema na kupata nafasi nyingi tu lakini haikuwa siku yetu''
Van Gaal alitua Old Trafford baada ya United kumaliza katika nafasi ya 7 katika ligi kuu ya Uingereza na amewanunua wachezaji wengu tu kwa gharama ya pauni milioni 131.7 akiwemo
mchezaji aliyegharimu kitita kikubwa zaidi katika ligi ya Uingereza Angel Di Maria aliyegharimu pauni milioni 59.7 alipotokea Real Madrid .
Kichapo hicho kwa kikosi kilichogharimu chini ya nusu milioni kukiweka pamoja ni ishara ya jinsi hali imezidi kudorora tangu aondoke kocha Alex Fergusson
0 comments:
Post a Comment