Katika michuano ya Diamond League ya jana usiku, Nijel Amos alimzidi
kasi ya kuufukuza upepo David Rudisha katika michuano ya mita 800 mjini
Zurich
Nijel Amos alimzidi nguvu David Rudisha
Mshindi huyo wa michuano ya Olympic David Rudisha alimaliza mbio zake
katika nafasi ya tatu kwenye mbio hizo za mita 800 wakati mwanariadha
mchanga na mwenye ubavu wa kutanua mapafu mbioni Nijel Amos kwa mara
ingine tena amejitwalia tena ubingwa huo wa mita 800
Na hii si mara ya kwanza kwa Amos kumshinda nguvu Rudisha kwani mwezi
uliopita katika michuano ya jumuiya ya madola maarufu kama Commonwealth
Games na kujitwalia medali ya dhahabu huku akitumia dakika 43. sekunde
77
Naye Ayanleh Souleiman alimshinda Rudisha na kutwaa nafasi ya pili kitendo kilichomlazimisha Rudisha kushika nafasi ya tatu
0 comments:
Post a Comment