Wanaume wanne waliokuwa wameshitakiwa kwa kosa la jaribio la kumuua aliyekuwa jasusi wa Rwanda Generali Faustin Kayumba Nyamwasa, nchini Afrika Kusini wamepatikana na hatia ya kosa hilo
Wawili kati ya sita walioshitakiwa wamefutiwa mashitaka
Nyamwasa alipigwa risasi na kujeruhiwa mwezi Juni mwaka 2010 nje ya nyumba yake mjini Johannesburg
Washukiwa wengine wawili akiwemo aliyekuwa dereva wake Nyamwasa,
walifutiwa mashitaka yao na hakimu Stanley Mkhari aliyetoa uamuzi wa
kesi hiyo
Nyamwasa alikimbilia nchini Afrika Kusini miezi kadhaa baada ya kukosana na aliyekuwa mshirika wake Rais Paul Kagame
Sady Abdou, Hemedi Denengo Sefu, Amani Uriwani, Richard Bachisa, Hassann
Nduli na Pascal Kanyandekwe, ndio wanaume sita waliokuwa wameshitakiwa
kwa kupanga njama ya kumuu Nyamwasa. Wote walikanusha madai hayo
Serikali ya Rwanda imekanusha madai ya kuhusika na jaribio la kumuua Nyamwasa
Hukumu dhidi yao itatolewa tarehe 10 mwezi Septemba.
Mwandishi wa BBC Nomsa Maseko anasema kuwa Nyamwasa alikuwa mahakamani kusikiliza kesi hiyo
0 comments:
Post a Comment