Taarifa za kutatanisha za kuibiwa kwa gari la ulinzi wa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta zimeibuka nchini humo
Msemaji wa serikali amekanusha madai kuwa gari lililoibiwa lilikuwa la ulinzi wa Rais
Taarifa hii ilitolewa na baadhi ya vyombo vya habari ingawa msemaji wa
Rais Kenyatta ameikanusha taarifa hiyo akisema kuwa gari lililoibiwa
lilikuwa la idara ya polisi likiendeshwa na inspekta mkuu wa polisi
Gari hilo lililokuwa lisemekana kuwa na uwezo wa kuhimili risasi,
liliibiwa usiku wa Jumatano na kwamba aliyekuwa analiendesha gari hilo
alikuwa afisa wa polisi
Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa Daily Nation
ikimnukuu mtu anayesemekana kuwa dereva wa gari hilo la kifahari
alilazimishwa kuvua nguo zake kabla ya kupokonywa gari hillo
Gari lenyewe lilikuwa na nambari ya usajili ya kibinafsi.
Ni gari la polisi au la Rais?
Kwa mujibu wa msemaji wa Rais, gari hilo aina ya
BMW 735 la mwaka 2000, lilikuwa linaendeshwa na inspekta wa polisi
alipovamiwa na wanaume wanne waliokuwa wamejihami karibu na eneo la Ruai
viungani mwa mji mkuu Nairobi.
Msemaji wa Rais Manoah Esipisu amekanusha madai
kwamba gari hilo lilikuwa moja ya magari ya ulinzi wa Rais Uhuru
Kenyatta kama ilivyokuwa imenukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari
Bwana Manoah amesema kuwa Inspekta aliyekuwa
anaendesha gari hilo aliporwa dola miasaba na simu yake gari hilo
lilipoibiwa saa tatu usiku. Alitekwa na majambazi hao kwa karibu saa
tano kabla ya kumwachilia usiku wa manane.
Alisema kuwa wezi hao walitoweka na gari hilo
ambalo alisema hutumiwa kwa shughuli za polisi na kwamba tayari msako
umeanzishwa ingawa gari hilo bado halijapatikana.
Kadhalika alikanusha kuwa gari hilo lilikuwa la ulinzi wa Rais na kwamba lenyewe lilikuwa na uwezo wa kuhimili risasi.
Visa vya wizi wa magari na utekaji wa madereva
sio jambo geni nchini Kenya ila kilichowashangaza wengi ni kwamba je
viopi gari la ulinzi wa Rais liibiwe?
Bwana Manoah amesema takwimu zinaonyesha visa
vya uhalifu vimepungua hasa katika jiji kuu Nairobi katika miezi ya hivi
karibuni na kwamba ulinzi unaendelea kuimarishwa.
0 comments:
Post a Comment