
Muonekano wa uwanja wa Simba sc uliopo eneo la Bunju jijini Dar es salaam
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
Imechapishwa Agosti 3, 2014, saa 7:35 usiku
TANGU
Simba sc ianzishwe miaka ya 1930’s haijawahi kulimika uwanja wake wa
mazoezi wala uwanja wa mazoezi ukilinganisha na Azam fc iliyoanza
kushiriki ligi kuu Tanzania bara kwa mara ya kwanza msimu wa 2008/2009
Hii
ni historia mbaya kwa klabu kubwa kama Simba ambayo wakati wa
kuanzishwa kwake ilikuwa inaitwa Queens, baadaye Eagles, Dar Sunderland
na mwaka 1971 ilibadilishwa jina na kuitwa Simba Sports Club.
Simba
yenye historia kubwa ya soka la Tanzania sasa ipo katika mchakato wa
ujenzi wa uwanja wake, lakini leo katika hotuba yake, Rais wa klabu
hiyo, Evans Elieza Aveva amewahakikishiwa wanachama wa Simba kuwa miezi
michache ijayo, klabu itamiliki uwanja wake wa mazoezi.
Uongozi
wa Ismail Aden Rage ulianza utekelezaji wa ujenzi wa uwanja wa mazoezi
eneo ya Bunju jijini Dar es salaam na sasa maendeleo ni mazuri ambapo
nyasi zilizopandwa na zinaendelea kuota.
Aveva alisema uongozi wake umetengeza zaidi ya shilingi milioni 600 ili kukamilisha ujenzi wa uwanja wa mazoezi.
Pia
Simba ipo katika mpango wa kujenga Hosteli za wachezaji ili kuepukana
na gharama kubwa wanazotumia kuwaweka wachezaji Hotelini.
0 comments:
Post a Comment