Mbwana Ally Samatta (kushoto) ameifungia bao la kufutia machozi Taifa stars
Na Baraka Mpenja
Imechapishwa Agosti 3, 2014, saa 12:14 jioni
HATIMAYE
safari ya timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars kuwania tiketi ya
kucheza fainali za mataifa ya Africa, AFCON 2015 nchini Morocco amefia
mikononi mwa timu ya taifa ya Msumbiji ‘Black Mambas’.
Taifa
Stars ikiwa ugenini katika dimba la Taifa la Zimpeto nje kidogo ya jiji
la Maputo imetandikwa mabao 2-1 katika mchezo wa marudiano wa kuwania
kupangwa hatua ya makundi ya kusaka tiketi ya AFCON mwakani.
Katika
Mechi ya kwanza iliyopigwa wiki mbili zilizopita jijini Dar es salaam,
vijana wa Mholanzi, Mart Nooij walitoka sare ya mabao 2-2 na leo hii
walihitaji kupata ushindi wa aina yoyote ile au sare ya kuanzia mabao
3-3.
Matokeo
ya jumla baada ya mechi mbili, Msumbiji wamefanikiwa kufunga mabao 4
na Taifa stars matatu, hivyo vijana wa Nooij kutupwa nje ya michuano kwa
wastani wa mabao 4-3.
Msumbiji
walikuwa wa kwanza kuandika bao la kuongoza dakika za mwisho za kipindi
cha kwanza kupitia kwa Josimar Tiago Machaisse, lakini Mbwana Ally
Samatta akaisawazishia Stars katika dakika ya 77.
Elias Pelembe ndiye 'mchawi' wa Taifa Stars kwa mwaka huu.
Dakika
ya 83, kiungo mshambuliaji wa Msumbiji, mzoefu, mwenye ujanja mwingi
wa kupiga chenga na kumiliki mpira, Elias Gasper Pelembe aliifungia
‘Domingues’ Msumbiji bao la pili na la ushindi.
Kihistoria Msumbuji wamemekuwa wababe wa Taifa Stars inapofika michezo ya mtoano, hasa kufuzu mataifa ya Afrika.
Mwaka
2007 Stars chini ya kocha Mbrazil, Marcio Maximo ilifungwa bao 1-0
katika mchezo wa mwisho jijini Dar es salaam kuwania kucheza fainali za
mataifa ya Afrika mwaka 2008 nchini Ghana na ingeshinda ingefuzu.
Bao
pekee la Msumbiji lilifungwa dakika ya za mapema kipindi cha kwanza na
aliyekuwa nahodha wake, Tiko Tiko akiunganisha kwa kichwa krosi nzuri
iliyochongwa kutoka winga ya kulia na Elias Pelembe.
Mwaka
2012 Taifa stars ilitolewa tena na Msumbiji kwa changamoto ya mikwaju
ya penati katika mchezo wa kuwania kucheza fainali za kucheza fainali za
mataifa ya Afrika mwaka 2013 nchini Afrika kusini.
Hatua hii ilifikia baada ya timu hizo kutoka sare ya bao 1-1 jijini Dar es salaam na kupata matokeo kama hayo mjini Maputo.
Kwahiyo Msumbiji bado wameendelea kuwa wababe wa Tanzania katika michezo ya mtoano.
Poleni sana Taifa Stars, Poleni Watanzania wote. Mipango mipya inatakiwa kuwekwa.
0 comments:
Post a Comment