Everton inataka kumsajili mshambulizi nyota kutoka Cameroon Samuel Eto'o kwa mkataba wa miaka 2
Mshambulizi huyo aliruhusiwa kuondoka Chelsea mwisho wa msimu uliopita
Liverpool pia walionesha niya ya kumsajili lakini mchezaji huyo hakuwahi ushindani kutoka kwa Mario Balotelli.
Kwa mujibu wa wandani huko Goodison ,huenda
mshambulizi huyo akashiriki mechi ya kufungua msimu baina ya Everton na
Chelsea siku ya Jumamosi
Everton tayari wamemsajili Romelu Lukaku kutoka Chelsea kwa
gharama ya pauni milioni £28m mbali na kumsajili Christian Atsu wa
mkopo.
Mshambulizi huyo ambaye aliwahi kuwa mchezaji nyota barani Afrika kwa miaka minne aliifungia Anzhi Makhachkala mabao 12 katika mechi 35 alizoshiriki
Mshambulizi huyo ambaye aliwahi kuwa mchezaji nyota barani Afrika kwa miaka minne aliifungia Anzhi Makhachkala mabao 12 katika mechi 35 alizoshiriki
Etoo aliwahi kuhudumu chini ya Mourinho akiwa Inter Milan
Alipokuwa Nou Camp, alitwaa ubingwa wa ligi ya Ulaya mara mbili katika mwaka wa 2006 na 2009 .
Eto'o alijiunga na Inter Milan 2009 kutokea Barcelona alipoisaidia kutwaa kombe la mabingwa chini ya Mourinho huko San Siro.
.
0 comments:
Post a Comment