Mabingwa wa ligi kuu ya Uingereza walifungua kampeini ya kutetea taji
lake kwa kuinyuka washindi wa pili msimu uliopita Liverpool mabao 3-1
katika uwanja wao wa nyumbani Etihad
Stevan Jovetic alipeleka kilio kwa Liverpool kwa kutikisa wavu mara mbili katika kila nusu.
Liverpool ambayo ilijitahidi kucheza vizuri katika kipindi cha kwanza
cha mchezo ilishindwa kutumia vizuri fursa ilizopata haswa katika
kipindi cha kwanza ilipobainika itambidi Kocha Brendan Rodgers kutafuta
mshambulizi mbadala baada ya kumuuza Luis Suarez.
Hata hivyo Rodgers atakuwa akitafuta ufufuo baada ya kumsajili mshambulizi wa Italia Mario Balotelli kwa pauni milioni 16 .
Uwanjani matumaini ya Liverpool kunusurika
kichapo yaliambulia patupu , Sergio Aguero sekunde 23 baada ya
kuchukua pahala pake Edin Dzeko.
Ushindi huo ni wa pili kwa kwa Man City msimu huu
Liverpool ilipata bao la kufutia machozi baada ya Pablo Zabaleta kujifunga mwenyewe katika dakika 20 za mwisho .
Liverpool itakumbuka Jovetic alipowahangaisha alipokuwa Fiorentina kwa ni jana ndiye aliyekuwa mwiba kwa safu yao ya ulinzi.
Meneja wa Manchester City, Manuela Pellegrini
amesema kikosi chake kilionyesha mchezo mzuri ambapo matunda yake ni
mabao matatu dhidi ya Liverpool.
Pellegrini anasema ni muhimu kujizolea pointi sita kutoka kwenye michezo miwili ingawa mwanzo ulikua mgumu kwao.
Kwa upande wake Rodgers atajiliwaza na hali ya
kuwa wamewasajili wachezaji wapya 9 msimu huu kwa hivyo bado anakisuka
kikosi chake kwa niya ya kutetea nafasi yao ya pili ama hata kuiboresha
nafasi hiyo ya msimu uliopita
.
0 comments:
Post a Comment