Marais wa Jumuia ya Maendeleo ya nchi za Mashariki na pembe ya Afrika
IGAD wanakutana leo mjini Addis Ababa Ethiopia kuujadili mzozo wa Sudan
Kusini.
Mzozo huo nchini Sudan Kusini utibuka mwezi Desemba wapiganaji wanaounga
mkono aliyekuwa makamu wa rais Riek Machar walipozua vita dhidi ya
Mejeshi ya Sudan Kusini mjini Juba
Maelfu ya watu wameuawa na wengine milioni moja nukta nane wamefurushwa
makwao tangu mapigano hayo kuzuka mwezi Desemba mwaka uliopita
Mkutano huu unawadia huku waasi wakishutumiwa vikali baada ya afisa
mmoja wa uchunguzi wa IGAD kuuwawa katika hali ya kutatanisha mjini
Bentiu
Miongoni mwa viongozi ambao tayari wamewasili jijini Addis Ababa
kuungana na mwenyeji wao Hailemariam Desalegn, ni rais wa Kenya Uhuru
Kenyatta, mwenzake wa Uganda Yoweri Museveni na Salva Kiir wa Sudan
Kusini
Mkutano huo ni juhudi ya hivi punde kutatua mzozo huo uliosababisha maafa mengi Sudan kusini.
Mazungumzo ya amani yanayoendelea jijini Addis Ababa, yamekwama kwa muda huku serikali ikisusia vikao kwa wiki kadhaa.
Aidha pande zote mbili zimeshutumiwa kwa kukiuka makubaliano ya
kusitisha mapigano yaliyotiwa saini mwezi Januari na Mei na pia
kushindwa kuafikia makataa ya Agosti kumi ya kubuni serikali ya mpito.
Rais Salva Kiir na aliyekuwa makamu wake Dkt Riek Machar wametofautiana kuhusu serikali hiyo ya mpito.
Igad imeonya kuwa huenda ikachukua hatua za
dhabu na kutangaza vikwazo dhidi ya viongozi wanaohujumu juhudi za
kupatikana amani nchini humo.
Lakini hii si mara ya kwanza kwa Igad kutoa onyo kama hilo.
Mwezi Machi baada ya mkutano mwingine wa marais
wa Igad, Mpatanishi mkuu wa mzozo huo Seyoum Mesfin alikuwa na onyo kama
hilo hilo
“ Mapigano yanaonyesha kwamba pande zote mbili hazina ari ya kumaliza vita.
NI ari yao ya kisiasa na ukakamavu ambao utamaliza vita hivi.
Kikao kimeweka bayana ujumbe wake, kwamba wakati huu ni lazima pande zote mbili ziitikie wito wa jamii ya kimataifa. “ alisema Mesfin
Wakati huohuo, Igad imeshutumu waasi nchii Sudan kusini baada ya mchunguzi wake mmoja kuuwawa.
Seyoum amesema waliohusika katika mauaji watachukuliwa hatua kali.
Mashirika ya misaada nayo yameonya kuwa nchini hiyo inakabiliwa na tishio la kiangazi huku vita vikitatiza utoaji wa chakula kwa mamilioni waliofurushwa makwao

0 comments:
Post a Comment