Muungano mmoja wa wanamgambo nchini Libya unasema kuwa umeuteka uwanja
wa ndege wa kimataifa wa Tripoli baada ya mapigano makali kati yake na
kundi pinzani la waasi
Picha zilizowekwa katika mtandao zimeonyesha wapiganaji hao wakisherehekea juu ya ndege na katika majengo ya uwanja huo.
Muungano huo unaoshirikisha wanamgambo wa
kiislamu pamoja na wanamgambo kutoka mji wa Misrata umesema kuwa
uliuteka uwanja huo licha ya mashambulizi ya angani yanayodaiwa
kutekelezwa na Misri pamoja na nchi za ufalme wa kiarabu.
Mwandishi wa BBC mjini Tripoli anasema kuwa kuna ripoti za kuendelea kwa vita kati ya makundi pinzani viungani mwa mji huo.
Uwanja huo umefungwa kwa takriban mwezi mmoja
sasa kufuatia vita kati ya makundi pinzani ya wanamgambo yaliozuka tangu
kuondolewa madarakani kwa aliyekuwa rais wa taifa hilo kanali Gaddafi
mwaka 2011.
0 comments:
Post a Comment