Posted by Williammalecela.com on Saturday, August 30, 2014
 |
"Tuna tatizo kubwa huko mitandaoni.
Tumefika hatua ya kuwapa umaarufu watu wenye matusi ya nguoni, wazushi,
wambeya, wanafiki. Wanaochafua wenzao, kutishia wenzao kwa kujifanya
askari JKT,JWTZ au hata Polisi kusengenya na kupost majungu.... Aina ya binaadamu
wanaostahili laana lakini twaishia kuwatukuza.
Kwenye hii mitandao,
matusi imekuwa njia ya mkato ya kupata umaarufu. Kuna wenzetu wengi tu
wenye 'umaarufu' huko Twitter, Facebook na Instagram lakini ukidadisi
chanzo cha 'umaarufu' huo, utaambiwa 'ah! huyu ana matusi si mchezo!'
Kuna watu wazima na akili zao wanatumia muda mwingi kwenye mitandao ya
kijamii aidha kunyanyasa wenzao kama si kusherehesha unyanyasaji huo.
Marehemu Betty ni victim wa yote hayo. Alitukanwa sana, na aliitwa
majina kadhaa ya kumdhihaki kabla ya kukutana na mauti. Kuna waliomwita
Di Maria, superstar uchwara n.k.. na ninaamini hao waliomuita hivyo
wanajifahamu na wengine wananisoma hapa." |
0 comments:
Post a Comment