Jeshi la Lesotho
Waziri mkuu nchini Lesotho Tom Thabane amekiambia Chombo cha Habari kwamba amelitoroka taifa hilo baada ya kupata vitisho vya maisha yake.
Akizungumza kutoka nchini Afrika kusini,Bwana
Thabane amesema kuwa vitenmdo vya jeshi nchini humo vimesitisha huduma
za serikali na kusababisha mapinduzi.
Awali Ripoti kutoka mji mkuu wa
maseru zilizsema kuwa jeshi lilizingira makao makuu ya polisi na kuzuia
matangazo ya radio pamoja na mtandao wa simu katika mji mkuu wa Maseru.
Uchaguzi uliozongwa na utata nchini humo miaka miwili iliopita ulisababisha kuundwa kwa serikali ya muungano isio dhabiti.
Licha ya mazungumzo ya kuleta amani mnamo mwezi
Juni ,hali ya wasiwasi ilitanda huku majirani wa taifa hiilo wakionya
dhidi ya mbinu yoyote isio ya kikatiba.
Taifa hilo limezungukwa na Afrika kusini na hutegemea sana jirani yake kwa masli asli pamoja na nafasi za kazi
0 comments:
Post a Comment