Alfonso Dhlakama
Kiongozi wa chama cha upinzani cha Renamo cha nchini
Msumbiji,Alfonso Dhlakama, ameonekana hadharani katika mji mkuu wa nchi
hiyo,Maputo, baada ya kuwa mafichoni zaidi ya miaka miwili.
Wanachama wa Renamo walionekana katika viwanja
vya ndege vya Maputo kumpokea kiongozi wao, wakiwa na bashasha na
nderemo kutokana na kumwona kiongozi wao hadharani.
Alfonso aliwasili Mjini Maputo akiwa ameambatana
na mabalozi kadhaa wanao wakilisha nchi zao Mozambique,ili
kumhakikishia usalama wake,ujio wa Alfonso umekuja mwezi mmoja tu baada
ya kusaini hati ya amani kumaliza harakati za vikundi vya wanamgambo wa
Renamo.
Alfonso anatarajiwa kuingia katika kinyang'anyiro cha kugombea nafasi ya uraisi katika uchaguzi unaotegemewa mwezi ujao
0 comments:
Post a Comment