Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba,Askofu Mstaafu, Donald Mtetemela , ambaye yuko katika Kamati Namba Nane ya Bunge, hilo amewashauri wajumbe wenzake kuwa suala la maadili na miiko ya viongozi na utumishi wa umma, lisiwe kwa watu hao tu bali hata kwa jamii nzima.
Kauli hiyo imetolewa leo na Askofu Mtetemela,wakati akichangia mjadala wa kujadili sura zilizobakia za Rasimu ya Katiba Mpya kwenye kikao cha thelasini na saba cha Bunge hilo linaloendelea mjini Dodoma, ambacho kinaendelea na sura ya Pili, Tatu, Nne na Tano za Rasimu hiyo.
Askofu Mtetemela aliyasema hayo akiwa anachangia mjadala katika Bunge hilo, katika sura ya Tatu ya Rasimu hiyo.
“Ninapenda kuunga mkono taarifa ya Kamati Namba Nne ya Bunge Maalum la Katiba ambayo ilibadilisha kichwa cha habari katika sura hii kuwa Maadili na Miiko ya Taifa. Neno maadili lina upana. Suala la maadili si kwa watawala tu, maadili yanaanza na jamii,” alisema Askofu Mtetemela.
Aliongeza kwamba kiongozi anatoka katika jamii, hivyo ni vema jamii lazima iwe maadili.
“Taifa lihimize jamii kuwa na utamaduni mzuri. Taasisi kujifunzia, vyuo vya elimu na vyombo vya dini vina wajibu wa kujenga maadili katika jamii,”alisisitiza.
0 comments:
Post a Comment