Posted by Williammalecela.com on Friday, September 12, 2014
 |
| Mhe. Mjenga akiwa katika picha ya pamoja na mwenyeji wake Mhe. Saeed Khoory. |
 |
Mhe. Omar Mjenga leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji
Mkuu wa kampuni ya mafuta ya ENOC ya Dubai, Mhe. Saeed Khoory pamoja na
uongozi wa juu wa kampuni hiyo.
Katika
mazungumzo, wamejadiliana njia za kuongeza uwekezaji wa kampuni hii
nchini Tanzania. Nia ni kuifanya Tanzania kuwa ofisi kuu ya Kanda ya
Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika.
Aidha,
Mhe. Mjenga amemuomba Mhe. Khoory kuona uwezekano wa kampuni hii kuajiri
Watanzania zaidi kuja kufanya kazi Dubai. Amekubali ombi hilo na
kuahidi kutoa maagizo kwa idara ya ajira kuorodhesha nafasi zilizopo ili
kuanza taratibu za kuajiri.
Kwa sasa, ENOC imekwishafungua ofisi zake Tanzania na wapo katika majadiliano na TPDC ili kujenga hifadhi maalum ya mafuta.
|
 |
| Picha ya pamoja na uongozi wa ENOC. |
 |
| Mazungumzo yakiendelea na uongozi wa ENOC. |
0 comments:
Post a Comment