Promosheni ya ‘Weka na Ushinde’ Iliyozinduliwa na Benki ya NMB ambayo itakushawishi wewe mteja kuweka fedha benki ili uweze kujipatia Zawadi Mbalimbali ambazo ni Bajaji,Bodaboda,Baiskeli na fulana za NMB tu bali pia faida kubwa ya riba Mara uwekapo fedha zako kwenye Benki ya NMBPromosheni hiyo hiyo itafanyika katika kipindi cha miezi mitatu kuanzi sasa mpaka Desemba 29,2014 na Inawahushisha Watanzania wote
Zawadi hizo zinathamani ya zaidi ya TZS 500 Milioni ambazo ni (Bajaji-52,Bodaboda-52,Baiskeli-400 na fulana-500).
Meneja wa Amana wateja-NMB Bw.Boma Raballak Akizungumza machache wakati wa Uzinduzi huo uliofanyika kwenye tawi la NMB Sinza Jijini Dar es salaam
Meneja Masoko wa NMB-Rahma Mwapachu Akizindua Rasmi Promosheni hiyo ambayo zawadi zenye dhamani ya Shilingi Millioni 500 Zitashindaniwa Kwa Kipindi cha miezi Mitatu
Meneja wa NMB kanda ya Dar es Salaam -Salie Mlay
Wateja wa NMB na Wasio wateja wanaweza kushiriki na nirahisi kwa mteja aliye na akaunti anahitaji kuweka Shilingi 50,000 kama kiwango cha chini na yule asiye na akaunti anahitaji kufungua akaunti NMB ili aweze kuweka aghalau TZS 50,0.00 kama kiwango cha chini ili aweze kuingizwa kwenye droo ya Bahati Nasibu.Naye Meneja wa Kanda jijini Dar es Salaam Salie Mlay amesema kwamba zawadi hizo zitatolewa kwenye matawi yote 150 yaliyopo nchini hii ni fursa kwa wananchi kuweza kufaidika na kampeni hiyo.
Zawadi hizo zitakuwa zikikabidhiwa kwa washindi mara moja kwa mwezi kupitia matawi mbalimbali ya NMB yaliyo kwenye kanda husika.
0 comments:
Post a Comment