Theodore Wafer
Jaji mmoja nchini Marekani
amemhukumu mwanamume mmoja kifungo cha miaka kumi na saba jela kwa kosa
la kumpiga risasi na kumuua mwanamke mweusi ambaye hakua na
silaha,ambaye alikua akigonga mlango mkuu wa nyumba yake mapema asubuhi.
Theodore Wafer,ambaye ni mzungu, alijitetea kua
alikua akihofia uhai wake ndipo akajitetea kwa kumpiga risasi binti huyo
mweusi aliyekua na miaka 19, Renisha McBride mjini Detroit.
Jaji huyo alimkinza Theodore kwa maamuzi yake
mabaya,lakini pia binti huyo hakustahili kufa.Binti Theodore alikua
nagonga katika nyumba hiyo kuomba msaa baada ya kupata ajali ya gari.
Baada ya kufanyia uchunguzi mwili wa binti huyo
walimkuta ana kiwango kikubwa cha pombe,mauaji ya binti huyo yalizusha
maandamano, na kifo chake kinafananishwa na kijana Andrew kutoka Florida
Trayvon Martin aliyepigwa risasi mwaka 2012
0 comments:
Post a Comment