Pesa zinazopora zinaweza kuwasaidia mamilioni ya watu katika mataifa yanayostawi
Inakisiwa dola Trilloni 1
huporwa kutoka kwa nchi maskini kila mwaka huku maisha ya mamilioni ya
watu katika nchi hizo yakihatarishwa.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa ripoti ya shirika la kupambana na umaskini la 'Organisation one'.
Shirika hilo linasema kwamba faida
zilizofikiwa katika kupambana na umaskini katika miongo miwili
iliyopita, zinakabiliwa na tisho kubwa kwa sababu ya viwango vya juu vya
ufisadi na uhalifu.
Matukio ya ufisadi ni pamoja na utumiaji wa makampuni ghushi na utengezaji wa pesa kwa njia haramu.
Ripoti hiyo inalaumu ufisadi kwa vifo vya watu milloni 3.6 kila mwaka.
Shirika hilo kadhalika linasema kwamba laiti
hatua zingechukuliwa kukomesha vyanzo vya ufisadi kukita mizizi na pia
kama mapato yaliyopatikana yangetumiwa kwa miradi ya afya - vifo vingi
vingeweza kuzuiwa kwa nchi zenye mapato ya chini.
Vile vile shirika hilo linanukuu kuwa ufisadi
unazidi kukithiri na kushinda majanga na maradhi yanayolemea mataifa
maskini duniani na hata kutaja matokeo ya ripoti yake kama kashfa ya
mabilioni ya dola.
Ripoti hiyo inanukuu: ''Ufisadi huzuia uwekezaji
wa sekta binafsi,kupunguza kasi ya kukuwa kwa uchumi,huongeza gharama
za kufanya biashara na inaweza kusababisha migogoro ya kisiasa.
Lakini katika mataifa yanayostawi, ufisadi ni
jinamizi kubwa. Wakati serikali inapokosa kupata rasilimali za kutosha
kuwekeza katika miradi yake ya afya, chakula, usalama,na miundo mbinu,
kutokana na ufisadi, gharama ya maisha hupanda na watoto ndio wenye
kuathirika zaidi.''
Shirika la One Organisation linasema kuwa iwapo ufisadi unaweza kutokomezwa katika mataifa ya kusini mwa jangwa la Sahara:
-Watoto wengine zaidi ya millioni kumi wataweza kupata elimu kila mwaka.
-Pesa za ziada zitapatikana ili kuwalipa walimu 500,000 wa shule za msingi
-Watu zaidi ya millioni 11 walioathirika na ugonjwa wa ukimwi wataweza kupata dawa za kupunguza makali ya Ukimwi.
0 comments:
Post a Comment