Thursday, September 11, 2014

 
Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’
MWENYEKITI
 wa Klabu ya Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ na katibu wake, William Mtitu wamefika pabaya kwa kudaiwa kushindwa kusalimiana huku kila mmoja akificha sura asikutane na mwenzake.
Tukio lililodhihirisha kuwa wawili hao hawaivi, lilichukua nafasi juzikati katika Viwanja vya Leaders Club vilivyopo Kinondoni jijini Dar, kulipokuwa na uzinduzi wa filamu iliyokwenda kwa jina la Mateso Yangu Ughaibuni. 
Wakati shamrashamra za uzinduzi zikiendelea, paparazi wetu aliwashuhudia wawili hao wakiombwa wapige picha kwa pamoja ambapo hakuna aliyekuwa tayari kutimiza zoezi hilo, wakachengana kwa kila mmoja kuchukua njia yake. 

Wakizungumza na paparazi wetu, baadhi ya mastaa walioshuhudia kituko hicho, walisema Steve Nyerere na Mtitu wanatakiwa wakae pamoja wamalize tofauti zao hata kama mmoja wao hatorudi katika kiti chake cha uongozi lakini kwa heshima waliyojijengea katika tasnia ya filamu hawapaswi kuwa na mabifu.SOMA ZAIDI>>

0 comments:

Post a Comment