Sexy lady wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Taarifa ikufikie kwamba sexy lady wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amemnasa aliyekuwa meneja wa Wema Isaac Sepetu, Martin Kadinda ambaye ndiye atakuwa meneja wake kwa sasa.Akizungumza na Amani kwenye Hoteli ya Hyatt Regency The Kilimanjaro iliyopo Posta jijini Dar hivi karibuni waliponaswa wamegandana kama ruba, Kadinda alimuwahi mwanahabari wetu na kumsihi kuwa hawana uhusiano wa kimapenzi bali kuna habari mpya.
Kadinda ambaye hivi karibuni alimwaga kibarua kwa Wema, alisema kwamba aliongozana na Lulu hotelini hapo kwa kuwa kulikuwa na Fainali ya Shindano la Miss Ilala, Dar, wakiwa ni mtu na meneja wake kama alivyokuwa kipindi yuko na Wema.
Martin Kadinda.


0 comments:
Post a Comment