Wakuu wa kandanda wa Sierra Leone wanasema mechi ijayo ya duru za mwanzo
za Kombe la Afrika, baina ya Sierra Leone na Ivory Coast, itafanywa
ingawa kuna ugonjwa wa ebola Afrika Magharibi
Shirika la Kandanda la Sierra Leone limesema itataja timu yao ambayo itakuwa na wachezaji walioko nje ya nchi.
Ivory Coast imesisitiza kuwa
haitaruhusu mechi hiyo kufanywa katika mji mkuu, Abidjan, kwa sababu ya
wasiwasi wa kutapakaza virusi vya ebola.
Lakini haikutangaza wapi mechi itafanywa na pengine inaweza kupoteza mechi hiyo.
Huku nyuma nchini Nigeria, mjane wa daktari
aliyekuwa mtu wa sita kufa kwa sababu ya ebola nchini humo, naye
ameonekana ameambukizwa virusi.
Na wagonjwa watatu wa daktari huyo mjini Port
Harcourt wamepelekwa katika zahanati maalumu lakini haikuthibitishwa
iwapo kweli wana virusi vya ebola.
0 comments:
Post a Comment