Waziri mkuu wa Lesotho Thomas Tabane
Msemaji wa waziri mkuu wa Lesotho,Thomas Thabane,amesema kua waziri mkuu
huyo atakutana na raisi wa Africa Kusini,Jackob Zuma mjini
Pretoria.Thabane alielekea nchini humo mwishoni mwa wiki,kwa mazungumzo
huku akilishutumu jeshi kwa jaribio la kutaka kumng'oa madarakani.
Africa kusini imetoa kauli kua jaribio lolote la kuipindua nchi hiyo
na kuvunja katiba halitavumilika.Naye mshauri wa karibu wa waziri huyo
kua anataka kupinduliwa si kweli,na waziri huyo anatarajiwa kurejea
nchini mwake ndani ya siku mbili zijazo.
Wachunguzi wa masuala ya kisiasa wanadai kua,
kumekua na majaribio ya kutaka kuipindua serikali tangu nchi hiyo
ilipojipatia uhuru wake mwaka 1966 na pia inakailiwa na machafuko ya
kisiasa miezi ya karibuni.
0 comments:
Post a Comment