
HATARI! Uwanja wa Ndege wa Mwanza si salama na unaweza kutumiwa na magaidi kama Al-Shabaab kuteka ndege na kuua watu wakati wowote, ushahidi mzito huu hapa.Jengo la Uwanja wa Ndege wa Mwanza. Upelelezi wa kina uliofanywa na gazeti hili bila kujulikana katika operesheni maalum iliyopewa jina la ‘HAKIKISHA NCHI SALAMA’, waandishi wetu waliokuwa jijini Mwanza walifanya jaribio la kutaka kuingiza bastola ndani ya ndege na kugundua ni jambo rahisi kuliko ilivyotarajiwa. Katika uchunguzi huo, ilibainika kuwa katika viwanja vyote Bongo, Uwanja wa Ndege wa Mwanza ndiyo rahisi kutumiwa na magaidi, hivyo kuna kila sababu ya mamlaka ya viwanja vya ndege nchini kuchukua hatua ili kunusuru maisha ya abiria na watu wengine.
Ni kawaida ya gazeti hili kufanya uchunguzi wa aina hii katika viwanja vya ndege na maeneo nyeti ili kuona kama hali ya ulinzi na usalama haiwezi kuruhusu vitendo vya kigaidi kufanyika.Miaka michache iliyopita, waandishi wetu walifanya jaribio katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar na kufanikiwa kuingia na bastola hadi ndani ya uwanja karibu kabisa na ndege ya rais bila kugundulika pamoja na ukaguzi mkubwa uliofanyika wakati wa kuingia.
Kwa Mwanza, uchunguzi umeonesha kuwa uwanja huo una eneo moja hatari ambalo mwenye nia ya kuingia na silaha ndani ya ndege anaweza kulitumia. Eneo hilo ni mlango uliopo kwenye jengo linalotazamana na maegesho ya magari karibu na mlango wa VIP.

Ofisi za Uwanja wa Ndege wa Mwanza ENEO LILIVYO
Mlango huo wa kioo upo kwenye jengo jipya la kusubiri abiria kupanda ndege (waiting lounge), umeandikwa ‘EXIT’ ukimaanishani ni wa kutokea wakati wa dharura.SOMA ZAIDI>>
0 comments:
Post a Comment