
MCHUNGAJI Peter Rashid Abubakari wa Kanisa la RGC lililoko Mbezi ya Shamba jijini Dar, amedaiwa kuoa mke wa pili aitwaye Pamela Didas Asenga akiwa na umri wa miaka 20 tu ‘dogodogo’. Mchungaji Peter Rashid Abubakari wa Kanisa la RGC akimuoa 'dogodogo', Pamela Didas. Kwa mujibu wa chanzo, ndoa hiyo ilifungishwa na Askofu Innocent Lugagi wa Kanisa la White House la Durban, Afrika Kusini, Agosti 29, mwaka huu.
Mke mwingine wa mtumishi huyo wa Mungu anaitwa Zuwena (Catherine) aliyemuoa mwaka 1985. Lakini kuna madai kwamba, mke huyo amemwacha.
“Alituambia Mungu amemfunulia na amempa mke mwingine mwema ambaye ni binti mbichi, watu wewee,” kilisema chanzo.
0 comments:
Post a Comment