Kituo cha polisi kilichopo ushirombo wilayani Bukombe mkoani Geita kimevamiwa na majambazi usiku wa saa tisa kuamkia leo huku askari wawili wakiuawa na watatu wakijeruhiwa vibaya
Ambapo taarifa za awali zinasema kuwa licha ya matukio hayo wamelipua chumba cha kuwekea silaha na zingine kuondoka nazo,pia wamefanikiwa kuondoka na bunduki zaidi ya 5 aina ya SMG na kutokomea nazo.
Watu wamekusanyika kituoni hapo kushuhudia huku kituo hicho kikiwa kimezungushiwa kamba nyekundu kwa kusitisha huduma na mahabusu waliokuwemo wamehamishwa.
Hata hivyo kamanda wa jeshi la polisi mkoani Geita Joseph Konyo yupo katika eneo la tukio kwa uchunguzi zaidi.
Tutawaletea taarifa kamili hivi punde, endelea kutembeleafarajimfinanga.com
0 comments:
Post a Comment