Mashabiki wa kilabu yasoka ya Gremio nchini Brazil
Mlinda lango mweusi ambaye
alibaguliwa kirangi katika mechi moja kubwa nchini Brazil amekataa
msamaha kutoka kwa mmoja ya mashabiki waliohusika na kitendo hicho.
Shabiki huyo wa kilabu ya Gremio ,Patricia
Moreira amepoteza kazi yake na kutishiwa maisha baada ya kuonekana
katika camera akimwita mchezaji huyo wa kilabu ya santos
,Aranha,Tumbili.
Amesema kuwa alitaka kukutana na mchezaji huyo
ili kumuomba msamaha binafsi,lakini Aranha amekataa ombi hilo akitaka
mashabiki waliohusika na kitendo hicho kuadhibiwa vilivyo.
Bi,Moreira amesema kuwa alilazimika kutoa
matamshi ya hayo ya ubaguzi wa rangi wakati timu yake ilipokuwa
ikishindwa katika mechi ya kuwania taji.
Kilabu ya Gremio imepigwa marufuku katika
mashindano hayo huku mashabiki ambao watajulikana walitoa matamshi hayo
ya kibaguzi wakipigwa marufuku ya kuona mechi za soka kwa miaka miwili.
0 comments:
Post a Comment