Wednesday, September 24, 2014

Bw. Abbas Abraham Afisa Mawasiliano na Bi Hawa Ladha Meneja Miradi endelevu wa Serengeti Beer wakizungumzia fursa za ufadhili  kwa wanafunzi zinaopati​kana na EABL Foundation. Fursa hii ya ufadhili ni mpaka 30th September 2014






SBL: WANAFUNZI KUPATA UFADHILI WA CHUO KWA 100%
DAR-ES SALAAM  22 September 2014.  Kampuni ya Bia  ya Serengeti (SBL) kupitia mradi wa  EABL foundation, mwaka huu tena imetoa ufadhili wa  masomo ya chuo kikuu kwa kugharamia  kwa asilimia 100 ikewemo karo, malazi  na fedha ya kujikimu kwa mwezi.

Mwaka huu, mradi utatoa ufadhili kwa somo ya michupuo shahada ya biashara, uhandisi, sayansi ya chakula, teknologia ya mawasiliano  na kompyuta kwa wanafunzi ambao wamefaulu kidato cha sita na hawana uwezo wa kujilipia.

Meneja Mradi  Endelevu Bi. Hawa Ladha alisema ufadhili huo ambao hufanyika mara moja kwa mwaka  ni  kwa  watanazania wanaotaka kusoma kwa vyuo vya  hapa nchini “Wanafunzi waliokizi vigezo vyote  vya kuomba ufadhili huo watawezeshwa  kusoma  na kufanikiwa katika malengo yao,” alisema

Meneja Hawa aliongeza ufadhili huo wa  kipekee ni kwa wanafunzi ambao wazazi wao hawana uwezo wa kuwalipia na akawashauri vijana kuchangamkia fursa hizo kwani  muda wakuomba haujaisha. Fomu za ufadhili  zinapatika katika tovuti ya www.eablfoundation.com na zimebaki siku kumi tu!
Maombi hayo ni lazima yambatanishwe  na barua ya wito ikionesha mojawapo ya michepuo  anaotaka kusoma, uthibitisho wa kuonyesha kuwa muombaji hana uwezo wa kifedha kwa ajili ya masomo, kuwasilisha  nakala ya vyeti cha kumaliza elimu ya  kidato cha sita na cha nne, fomu ya maombi iliyojanzwa  barua ya kukubaliwa masomo ya chuo kikuu.
Pia Wanafunzi  ambao hawajapata barua za kujiunga  chuo kikuu  lakini wanasifa za kujiunga wanaruhusiwa kuomba. Kwa taarifa zaidi wanafunzi wameshauriwa kutumia mitandao ya kijamii kwa kutembelea tovuti ya www.eablfoundation.com

Mradi huu wa EABL Foundation ulianza ufadhili kwa wanafunzi wa chuo tangu mwaka 2005 na wanafunzi waliomaliza wapo zaidi ya 200 kutoka Afrika Mashariki.  Hapa Tanzania Zaidi ya wanfunzi 26 wameshapat ufadhili huu na wanfanya kazi katika kampuni mbalimbali.

Mradi wa EABL foundation hutumia milioni 39,600,000 kila mwaka kufadhili wanafunzi wa chuo.Had sasa wameshatumia bilioni 316,800,000 kwa miaka nane.
 

0 comments:

Post a Comment